

Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ameuelekeza uongozi wa kituo cha afya cha Buguruni kuzibiti mianya ya upotevu wa fedha katika kituo hicho ili kuendelea kuboresha miundombinu ya kituo na kufanikisha utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo mara baada ya kutembelea na kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika kituo cha afya cha Mnazi Mmoja na kituo cha afya cha Buguruni.
“tunapolenga upatikanaji wa huduma za afya kwa ubora zaidi lazima tuthibiti mianya ya upotevu wa fedha na Kuongeza mapato Kwa kutoa huduma bora Kwa wateja wetu” amesisitiza
Aidha, Dkt. Mfaume ametaka timu ya usimamizi wa huduma za Afya (CHMT) katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Kuongeza usimamizi wa fedha katika kituo vituo mbalimbali katika Halmashauri hiyo.
Pia Dkt. Mfaume ameielekeza timu ya Usimamizi wa huduma za Afya (CHMT) kushirikishana na Viongozi wa Serikali za Mitaa ili kufanikisha utoaji wa huduma chanjo Kwa Watoto katika Halmashauri hiyo.






Post a Comment