Na Mapuli
Kitina Misalaba
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, ameendesha mkutano
wa hadhara kwa ajili ya kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano waliompa tangu
achaguliwe mwaka 2020, huku akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa
kipindi cha miaka minne iliyopita kuelekea mwisho wa kipindi chake cha miaka
mitano.
Katika taarifa hiyo, Mhe. Zamda
amesema kata ya Ndala imepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali zikiwemo elimu, miundombinu, afya, TEHAMA, umeme,
mikopo kwa vikundi, na upimaji wa ardhi, akiahidi kwamba kwa siku chache
zilizobaki, hatamaliza muda wake bila kukamilisha changamoto zilizobaki.
Amesema kuanzia mwaka 2021 hadi
Februari 2025, idadi ya wanafunzi katika shule ya Msingi Msufini na Ndala
Sekondari imeongezeka kwa asilimia 100 kutokana na utekelezaji wa Mpango wa
Elimu Bila Malipo. Aidha, ufaulu kwa wanafunzi wa Ndala Sekondari umeongezeka
kutoka 97% mwaka 2023 hadi 98% mwaka 2024, hatua iliyofanikisha shule hiyo
kupokea wanafunzi wengi na kushika nafasi ya juu katika Manispaa.
Zaidi ya shilingi milioni 276
zimetumika katika miradi mbalimbali ya elimu kama ifuatavyo:
Ndala
Sekondari
- Maabara ya Sayansi (2021) – Tsh 30 milioni
- Ukamilishaji darasa (nguvu za wananchi) – Tsh 5.42
milioni
- Vyoo 12 – Tsh 13.2 milioni
- Vyumba 2 + ofisi na samani (2022) – Tsh 40 milioni
- Vyumba 4 + samani (2023) – Tsh 80 milioni
Shule ya Msingi
Msufini
- Darasa (nguvu za wananchi) – Tsh 15 milioni
- Vyumba 3 + samani (2023) – Tsh 78 milioni
- Vyoo 3 – Tsh 6.6 milioni
Shule ya Shikizi
Msufini B
- Vyumba 2 + ofisi (hatua ya lenta, nguvu za wananchi na
mfuko wa jimbo) – Tsh 9.3 milioni
Zamda
ameeleza kuwa kata ya Ndala imenufaika na miradi mingi ya barabara kwa
kipindi cha miaka minne. Hadi sasa, barabara kadhaa zimetengenezwa kwa
kuchongwa, kujengwa mitaro na makalavati katika mitaa ya Banduka, Mwabundu,
Mlepa, Ndala, Mapinduzi na maeneo mengine, ikiwa ni pamoja na:
- Ujenzi wa daraja la Ndala – Mwasele: Tsh 103.2 milioni
- Ujenzi wa mitaro na makalavati mbalimbali: Zaidi ya Tsh
80 milioni
Amesema kupitia mpango wa mikopo ya Halmashauri, kikundi cha watu
wenye ulemavu kiitwacho I CAN kilipatiwa mkopo wa Tsh milioni 20 kwa
ajili ya kujikwamua kiuchumi.
Diwani huyo ameeleza kuwa mtaa wa
Mlepa tayari umeunganishwa na umeme, huku mtaa wa Ndala upo kwenye hatua za
kusimikwa kwa nguzo na kufungwa nyaya.
Zaidi ya viwanja 3,262 vimepimwa
kwenye mitaa mbalimbali:
- Mlepa: Viwanja 1,050
- Mwabundu: Viwanja 1,212
- Ndala: Zoezi la kupima na kugawa namba linaendelea
Kata hiyo haikuwa na kituo cha afya
tangu 2020, lakini mwezi Januari 2025 eneo limepatikana na wamiliki wote
wamelipwa fidia. Ujenzi wa kituo cha afya unatarajiwa kuanza mwaka 2026.
Kata ya Ndala sasa ina watendaji
katika kila mtaa isipokuwa mmoja ambao nao unatarajia kupata mtendaji muda
wowote. Idara ya elimu pia imeongezewa walimu, hali iliyoboreshwa zaidi na
ajira za serikali zinazoendelea.
Katika hatua nyingine, Kata ya Ndala
imefungua soko la kisasa lililowekewa mageti kwa Tsh milioni 5. Pia, gulio
jipya limeanzishwa linalofanyika kila Jumatano, likihudumia wakazi wa Ndala na
maeneo jirani.
Amesema shule ya Sekondari Ndala imepata kompyuta 2 na printa kwa
ajili ya elimu ya TEHAMA. Ofisi ya kata nayo imenunua kompyuta moja ambayo
imerahisisha utoaji wa huduma na uandaaji wa taarifa.
Wakizungumza baada ya mkutano huo,
baadhi ya wananchi wa Ndala wamepongeza kazi kubwa ya maendeleo iliyofanyika,
huku wakimuomba Mhe. Zamda kuhakikisha changamoto zilizobaki zinamalizwa kwa
wakati.
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye
mkutano wake wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akiwashukuru wananchi.





Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye
mkutano wake wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye
mkutano wake wa hadhara.

Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye
mkutano wake wa hadhara.
Wananchi wa kata ya Ndala wakifuatilia mkutano wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye
mkutano wake wa hadhara.
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban, akizungumza kwenye
mkutano wake wa hadhara.
Post a Comment