" JAMII YA KIFUGAJI KUTOKA KATIKA KABILA LA MASAI WAPATA MAFUNZO YA UFUNGAJI NYUKI

JAMII YA KIFUGAJI KUTOKA KATIKA KABILA LA MASAI WAPATA MAFUNZO YA UFUNGAJI NYUKI


Na,Lucas Raphael ,Tabora 
 
Jamii ya kifugaji kutoka katika kabila la masai wanaoishi ndani ya Tarafa ya Loliondo iliyopo Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha wameiomba Serikali kuwawezesha vifaa vya kisasa vya kufugia na kuchakata mazao ya Nyuki.
 
 
Lengo likiwa kuwajengea uwezo ili  waweze kuondokana na adha ya kutumia vifaa duni katika kuchakata mazao ya Nyuki na kujikwamua kiuchumi pamoja na kuendana na masoko ya kitaifa na kimataifa.
 
 
 
Kauli hiyo ilitolewa na Mfugaji wa Nyuki Noorkishili Kukutia wakati wa kuhitimu mafunzo ya  muda mfupi  ya ufugaji Nyuki ambayo yamefanyika katika Chuo cha ufugaji Nyuki  mkoani Tabora.
 
 
Alisema kwamba lengo la kupatiwa vifaa Bora vinavyoendana na ukuaji wa Teknolojia katika ufugaji huo na namna itakavyochangia kukuza pamoja na kuongeza ubora wa Zao hilo.
 
 
 
 
Alisema kwamba mafunzo hayo  yalilenga kuwajengea ujuzi wa kisasa katika ufugaji wa nyuki na kupewa mbinu bora za utunzaji wa mazingira pamoja na kuongeza tija ya uzalishaji wa zao hilo.
 
 
Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Shirika la Frank Foot Zoological Society(FZS),  Veronika Mtoka alisema kwamba ni muhimu jamii kushiriki katika shughuki za utunzaji wa mazingira lengo likiwa ni kupatia mbinu mbala kuachana na ufugaji na kuingia kwenye ufungaji wa nyuki kwa ajili ya kutunza mazingira .
 
Afisa Maendeleo wa kata ya Oloipiri,wilaya ya Ngorongoro mkoni humo  Lilian Mbunito alisisitiza umuhimu wa jamii kushiriki katika shughuli endelevu zinazochangia kuongeza kipato pasipo kuathiri mazingira.
 
Alisema kwamba wafugaji hao wapo 23 kati yao wanaume ni 13 na wanawake 10 washiriki hao no wanachama wa Vikundi vya COCOBA (Conservation Community Bank )iliyopo wilayani. Humo.
 
Veronika alisema kwamba Vikundi hivyo vinajishughulisha na uwekaji wa Akiba ,kukopeshana ,Ubofadhi mazingira pamoja na ufugaji nyuki na mifugo.
 
Mafunzo  ya muhimu katika kuboresha sekta ya ufugaji wa nyuki nchini Tanzania,kwa kuwa yanalenga kuinua Maisha ya jamii kupitia shughuli rafiki kwa mazingira zinazoweza kuwanufaisha kiuchumi kwa muda 
Mwisho  





Post a Comment

Previous Post Next Post