Majina ya Waliochaguliwa Kidato cha Tano, Form Five Selection
Wanafunzi 149,818 sawa na asilimia 69.96 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano, huku 64,323 wakichaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu.
Jumla ya wanafunzi 214,141 wakiwemo wasichana 97,517 na wavulana 116,624 ilibainishwa wana sifa za kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi ikijumuisha wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalumu.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa ameyasema hayo leo Juni 6, 2025 wakati akizungumzia kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo mbalimbali.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya elimu ya ufundi mwaka, 2025 inapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais -Tamisemi ya www.tamisemi.go.tz na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi www.nactvet.go.tz.
Post a Comment