" LEMA AZUIWAUHAMIAJI WATOA UFAFANUZI TUHUMA ZA LEMA

LEMA AZUIWAUHAMIAJI WATOA UFAFANUZI TUHUMA ZA LEMA


 



Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media 

Idara ya Uhamiaji ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitisha kumzuia  Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo "CHADEM" Godbless Jonathan Lema kutoka nchini na kushikilia pasipoti yake ya kusafiria huku ikimtaka Lema kuripoti katika ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Taarifa hiyo imetolewa leo  06, 2025 na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, SSI. Paul J. Mselle imeeleza kuwa Lema amezuiliwa leo tarehe 6 Juni, 2025 katika kituo cha uhamiaji cha mpaka wa Namanga Mkoani Arusha na kubainisha kuwa utaratibu uliotumika kumzuia kutoka nchini ni wa kawaida na unatumika kwa raia yeyote pale ambapo Idara imepata taarifa zinazohitaji mhusika kuhojiwa.

“Aidha,Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za uongo zilizochapishwa na ndg. Lema kupitia mitandao ya kijamii kuwa zuio hilo linawalenga viongozi wote wa CHADEMA."

Amesema msemajai mkuu wa uhamiaji  katika  sehemu ya taarifa hiyo.



Post a Comment

Previous Post Next Post