" JESHI LA POLISI KUWASHUGHULIKIA WATAKAOPANGA KUVURUGA AMANI

JESHI LA POLISI KUWASHUGHULIKIA WATAKAOPANGA KUVURUGA AMANI




Jeshi la Polisi nchini limewahakikishia wananchi kuwa, lipo imara na litahakikisha linadhibiti vitendo vya kihalifu kwa mujibu wa sheria na halitakuwa na muhali na mtu ama kikundi chochote kitakachopanga au kutakakujaribu kuvuruga amani ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Juma Haji wakati akihitimisha mafunzo ya medani za kivita kwa wanafunzi wa kozi ya Uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi katika kambi ya Polisi iliyopo Mkomazi mkoani Tanga Mei 24,2025.

Kamishna Awadhi amewataka wanafunzi hao kuyatumia kwa usahihi mafunzo hayo kwenye maeneo yao watakayopangiwa ili kutatua changamoto mbalimbali hasa za kihalifu zilizopo kwenye jamii.

Naye Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Mambosasa amesema kuwa, askari hao wa kozi ya Uafisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ikiwemo namna sahihi ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu na namna ya kutoa huduma bora kwa mteja.


Post a Comment

Previous Post Next Post