" KIBATALI 'Kesi ya Tundu Lissu Mahakama Imekubali Mapingamizi Yetu Leo'

KIBATALI 'Kesi ya Tundu Lissu Mahakama Imekubali Mapingamizi Yetu Leo'

 KIBATALI 'Kesi ya Tundu Lissu Mahakama Imekubali Mapingamizi Yetu Leo'


Wakili Peter Kibatala, ambaye ni miongoni mwa Mawakili wanaomtetea Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu kwenye kesi zake zinazoendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam amesema maamuzi ya Mahakama kukubaliana na mapingamizi yao na kuagiza mteja wao aletwe Mahakamani kusomewa maelezo ya awali ya kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uwongo kwenye mtandao wa YouTube ni ya kushujaa na yanayolinda heshima ya muhimili huo wa dola


Akizungumza na wanahabari kwenye viunga vya Mahakama hiyo leo, Jumanne Mei 06.2025 Wakili Kibatala ametoa wito pia kwa wananchi watakaohudhuria shauri hilo siku za usoni kuwa watulivu na kuhakikisha wanafuata miongozo ya Mahakama, katika maamuzi ya mapingamizi hayo Mahakama imetoa maelekezo yafuatayo:


(i) Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam itasikiliza preliminary hearing (PH) katika Mahakama ya wazi (open court), yaani mtuhumiwa atakuwa Mahakamani moja kwa moja,


(ii) Mahakama itasikiliza preliminary hearing (PH) katika open court namba 1 siku ya tarehe 19.05.2025,


(iii) Maafisa wa Jeshi la Magereza na Jamhuri kwa ujumla wanalazimika kumleta mtuhumiwa Mahakamani na umma (wananchi) wataruhusiwa kufika Mahakama ya wazi kusikiliza bila kikwazo chochote,


(iv) Mahakama inaomba umma (wananchi) kuwa na utulivu na kuzingatia kanuni za usalama katika eneo la Mahakama siku ya kesi, na


(v) Mahakama hiyo pia imeamuru na kutoa maagizo yote yaliyotajwa kufuatwa na kuzingatiwa bila dosari yoyote.

Post a Comment

Previous Post Next Post