

Mkurugenzi wa Gold FM, Bi. Neema Mghen, akipokea
cheti cha pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala
Mlolwa, kwa mchango wake katika maendeleo ya wanawake kupitia jukwaa la
Mwanamke Chuma na harakati mbalimbali za kijamii.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani,
pamoja na Mkurugenzi wa Gold FM, Bi. Neema Mghen, wametunukiwa vyeti maalum
vya pongezi kutokana na mchango wao mkubwa katika kuwawezesha wanawake kiuchumi
na kijamii.
Vyeti hivyo vimetolewa katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa
la Wanawake Halmashauri ya Ushetu, iliyofanyika katika kata ya Ulowa, ambapo
viongozi hao wametambuliwa kwa kuwa mstari wa mbele katika kubuni na kuunga
mkono majukwaa yanayoongeza thamani ya mwanamke katika sekta mbalimbali.
Mhe. Cherehani ametambuliwa kwa juhudi zake za
kisera na ufuatiliaji wa fursa za kiuchumi kwa wanawake wa Ushetu, huku Bi.
Neema akipewa heshima hiyo kutokana na mchango wake kupitia jukwaa la Mwanamke
Chuma, ambalo linaendelea kuwa sauti ya mwanamke katika nyanja mbalimbali za
maendeleo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa serikali,
vyama vya siasa, pamoja na wanajamii waliojitokeza kuunga mkono juhudi za
kuinua wanawake katika wilaya hiyo.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akimkabidhi cheti chake Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Mhe. Emmanuel Cherehani, kutokana na mchango wake katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia sera na juhudi za maendeleo katika jimbo lake.
Mkurugenzi wa Gold FM, Bi. Neema Mghen, akiwashukuru
Wanawake kwa kutambua mchango wake huku akiwaomba kuendelea kuchangamkia fursa
zinazojitokeza katika jamii.
Post a Comment