" WAFANYAKAZI GOLD FM WANG'ARA KATIKA MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2025

WAFANYAKAZI GOLD FM WANG'ARA KATIKA MAADHIMISHO YA MEI MOSI 2025

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi cheti kwa Steve Kanyefu wa Gold FM, kama Mtangazaji Bora kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani – Mei Mosi 2025.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akimkabidhi cheti kwa Emmanuel Mlelekwa wa Gold FM, kama Mwandaaji Bora wa Vipindi katika maadhimisho ya Mei Mosi 2025.


Na Mapuli Kitina Misalaba

Wafanyakazi wa Kituo cha Redio cha GOLD FM kilichopo Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga wameibuka kidedea katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, baada ya kutunukiwa vyeti na zawadi za Laptop kwa kutambua mchango wao katika tasnia ya utangazaji.

Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Usafirishaji (Communication and Transport Workers Union) COTWU imewatuza wafanyakazi hao kwa kazi nzuri na ubunifu mkubwa waliouonesha katika uandaaji wa vipindi pamoja na utangazaji wenye weledi na mvuto kwa jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ndiye aliyekabidhi vyeti hivyo wakati wa maadhimisho hayo, ambapo Mtangazaji Steve Kanyefu ametunukiwa Cheti cha Mtangazaji Bora, huku Emmanuel Mlelekwa akikabidhiwa Cheti cha Mwandaaji Bora wa Vipindi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka COTWU, zawadi za Laptop tayari zimewasilishwa kwa Uongozi wa Gold FM ili zikabidhiwe rasmi kwa wahusika hao waliong’ara.

Hatua hiyo imetajwa kuwa chachu ya kuongeza ari na ubunifu kwa wafanyakazi katika sekta ya utangazaji huku ikitambua mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo ya jamii.

Gold FM Tanzania, chombo cha habari kinachozidi kung'ara kanda ya ziwa na mikoa jirani, hupeperusha matangazo yake kupitia masafa yafuatayo:

📻 88.7 Kahama
📻 88.7 Shinyanga
📻 94.5 Geita
📻 90.7 Simiyu
📻 94.5 Mwanza
📻 102.5 Tabora
📻 106.5 Kagera
📻 88.5 Mara
📻 102.1 Kigoma

Kupitia masafa haya, Gold FM imekuwa daraja la taarifa, burudani na elimu kwa mamilioni ya wasikilizaji nchini Tanzania – ikitangaza kwa weledi na ubunifu unaotambulika hadi ngazi za kitaifa kama ilivyoonekana katika maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu.

Steve Kanyefu (Mtangazaji Bora) na Emmanuel Mlelekwa (Mwandaaji Bora wa Vipindi) wa Gold FM.






 

Post a Comment

Previous Post Next Post