" MISA TAN, WAN IFRA NA THRDC WAANDAA MKUTANO KUJADILI UHIMILIVU WA VYOMBO VYA HABARI DAR ES SALAAM

MISA TAN, WAN IFRA NA THRDC WAANDAA MKUTANO KUJADILI UHIMILIVU WA VYOMBO VYA HABARI DAR ES SALAAM

 Na  Mwandishi wetu - Dar es salaam


Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA Tan) Kwa kushirikiana na Taasisi ya WAN IFRA pamoja na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) wameandaa mkutano wa Wakuu wa Vyombo vya habari vya Jijini Dar es salaam kujadili uendelevu na uhimilivu wa Vyombo vya habari.

Mwenyekiti wa MISA Tan, Edwin Soko amesema, mkutano huo unalenga kuibua changamoto za  uwekezaji kwenye Vyombo vya habari na kujadili Nini kifanyike ili Vyombo hivyo viweze kuwa na uendelevu.

Naye Mgeni Rasmi Bwana Onesmo Orengurumwa amesisitiza kuwa vyombo vya habari viwe na utaratibu wa kutengeneza ajenda zenye mashiko kwenye kuleta maendeleo tofauti na sasa kwa jamii ndio inaelekeza nini kifanyike kwenye Vyombo vya habari.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa wamiliki wa Vyombo vya habari ,Samweli  Nyala amesema kuna umuhimu wa kujadili kwa pamoja changamoto za uwekezaji wa Vyombo vya habari ili kupata suluhisho la pamoja.

Kwa upande wa washiriki wametoa michango mbalimbali ya namna ya kukabiliana na changamoto za uwekezaji kwenye sekta ya habari.

Mkutano huo ni wa siku moja na umefanyika kwenye Hotel ya Four Point Jijini Dar es salaam.   

Post a Comment

Previous Post Next Post