" Mwabukusi: Tunamtaka Mdude Akiwa Hai

Mwabukusi: Tunamtaka Mdude Akiwa Hai

 Mwabukusi: Tunamtaka Mdude Akiwa Hai


Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniphace Mwabukusi, amevitaka vyombo vya dola kuhakikisha kuwa mwanaharakati Mdude Nyagali anapatikana akiwa hai, huku akilaani vikali kauli ya kutolewa zawadi ya Shilingi milioni tano kwa atakayesaidia kupatikana kwake akiwa hai au mfu.


“Tumesikia na kuona maafisa wa polisi kutoka Makao Makuu wakishughulikia suala la Mdude, lakini pia tumeshuhudia tangazo lililosambazwa mitandaoni kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiahidi zawadi ya Shilingi Milioni Tano kwa atakayefanikisha kupatikana kwa Mdude – eti akiwa hai au amekufa. Hili haliingii akilini,” amesema Mwabukusi kupitia chapisho lake katika mtandao wa X siku ya Jumanne.


Amesisitiza kuwa Mdude siyo jambazi, mwizi wala mhalifu wa kawaida, bali ni mwanaharakati ambaye adui zake wakuu ni wale wasio na uvumilivu wa kukosolewa.


“Msimamo wetu kama Rafiki za Mdude ni mmoja: Tunamtaka Mdude akiwa hai. Kama kuna kosa lolote, ashitakiwe kwa mujibu wa sheria. Hatuwezi kuvumilia taifa linalogeuka kuwa la mateso na vitisho kwa wanaoikosoa serikali,” ameongeza.


Aidha Mwabukusi ametahadharisha kuwa uvumilivu wa wananchi unafikia ukingoni, na kama ukweli kuhusu kupotea kwa Mdude hautatolewa haraka, hatua kali zaidi zitachukuliwa.


“Tunaendelea kujitahidi kuwa na hekima kabla ya kufikia ukomo wake. Bila Mdude na majibu yanayoeleweka kuhusu nani anawateka Watanganyika, punde tutafikia mahali pa kuchora mstari na kutafuta suluhisho mikononi mwetu. Mungu atakuwa upande wetu, Katiba itakuwa upande wetu, sheria itakuwa upande wetu, na jumuiya za kimataifa zitakuwa upande wetu”, ameeleza huku akimalizia kwa maneno yenye hamasa kubwa: “Sisi siyo njiwa tunduni, sisi ni tai kichaa.”


Siku ya Jumatatu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Juma Homera alisema kuwa tayari amelielekeza Jeshi la Polisi kuongeza jitihada za kuwatafuta wahusika waliomshambulia kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mdude Nyagali, huku akiahidi Tsh Milioni 5 kwa atakayesaidia kumpata kada huyo alipo akiwa hai au amekufa.


Akizungumza baada ya viongozi wa CHADEMA mkoani humo na Kanda ya Nyasa kufika ofisini kwake kujua hatua zilizochukuliwa, Dkt. Homera alisema yupo pamoja na chama hicho kuhakikish

Post a Comment

Previous Post Next Post