" Profesa Yakub Janabi, Ashinda Kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Profesa Yakub Janabi, Ashinda Kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

 

Profesa Yakub Janabi, Ashinda Kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
Profesa Yakub Janabi, Ashinda Kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

BREAKING: Profesa Yakub Janabi, Ashinda Kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO)

Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Masuala ya Afya na Tiba, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Yakub Janabi, ametangazwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) – Kanda ya Afrika baada ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliofanyika Mei 18, 2025, mjini Geneva, Uswisi.

Uchaguzi huo umefanyika kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa WHO-Kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile, aliyefariki dunia kabla ya kuanza rasmi majukumu yake.

Katika uchaguzi huo, Prof. Janabi aliwakilisha kanda ya Afrika Mashariki na alikuwa mgombea pekee kutoka nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, akiwania nafasi hiyo dhidi ya wagombea wengine wanne waliotoka Afrika Magharibi. Wagombea waliokuwa naye kwenye kinyang’anyiro hicho ni Dkt. N’da Konan Michel Yao kutoka Ivory Coast, Dkt. Dramé Mohammed Lamine kutoka Guinea, Dkt. Boureima Hama Sambo kutoka Niger na Prof. Mijiyawa Moustafa kutoka Togo

Ushindi wa Prof. Janabi umetokana na maandalizi makini ya Tanzania kupitia Ujumbe Maalum ulioongozwa na Waziri wa Afya Tanzania Bara, Jenista Mhagama, na Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Mazrui, ukishirikiana na Kamati ya Uchaguzi iliyoongozwa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Viongozi hao walifanya kampeni thabiti kuanzia ngazi ya mawaziri, mabalozi hadi washirika wa maendeleo, wakimnadi Prof. Janabi kama mgombea mwenye uwezo mkubwa, tajriba pana ya kitaifa na kimataifa, pamoja na maono ya kuimarisha huduma za afya barani Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post