Na Mapuli Kitina Misalaba
RS Berkane ya Morocco imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kwa mara ya tatu katika historia yao, baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Simba SC ya Tanzania kwenye mchezo wa marudiano wa fainali.
Mchezo huo wa pili umechezwa Mei 19, 2025, huku RS Berkane wakilinda ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliopigwa Morocco. Kwa matokeo ya jumla ya mabao 3-1, RS Berkane wametawazwa mabingwa wa michuano hiyo kwa msimu wa 2024/2025.
Simba SC waliingia katika mchezo wa marudiano wakiwa na matumaini ya kufanya kile kinachoitwa "comeback", lakini juhudi zao hazikutosha kugeuza matokeo dhidi ya wakali hao wa Kaskazini mwa Afrika.
Ushindi huu unaifanya RS Berkane kujiimarisha zaidi katika ramani ya soka la Afrika, huku wakiweka historia nyingine ya mafanikio katika michuano ya CAF.

Post a Comment