Sheikh wa Mkoa wa
Shinyanga, Ismail Makusanya, akikata utepe ikiwa ni sehemu ya kuzindua Msikiti
mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata
ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.
Na
Mapuli Kitina Misalaba
Sheikh wa Mkoa wa
Shinyanga, Ismail Makusanya, amezindua rasmi Msikiti mpya unaoitwa Masjid
Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili,
Manispaa ya Shinyanga.
Msikiti
huo umejengwa na taasisi isiyo ya kiserikali JAMIIYAATULI AKHLAAQUL ISLAAM (JAI) kwa gharama ya Shilingi
Milioni 50 hadi kukamilika, ambapo uzinduzi wake umefanyika leo Mei 9, 2025 baada
ya Swala ya Ijumaa na kuhudhuriwa na waumini pamoja na viongozi mbalimbali wa
dini na kijamii.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Sheikh Makusanya ameipongeza JAI kwa kujitolea na kusogeza
huduma za kiroho karibu na wananchi, akisema kuwa hatua hiyo ni mfano wa kuigwa
na wadau wengine wa maendeleo.
"Ni
muhimu kwa taasisi na watu binafsi kuendeleza moyo wa kujitolea kama
ilivyofanywa na JAI, ili kuimarisha maendeleo ya dini na jamii kwa
ujumla," amesema Sheikh Makusanya huku akisisitiza umoja na mshikamano
katika kutekeleza shughuli za maendeleo.
Ameihakikishia
JAI kuwa Mkoa wa Shinyanga uko tayari kushirikiana na taasisi hiyo katika
kufanikisha malengo yake kwenye sekta ya dini na huduma za kijamii.
Kwa
upande wake, Amili wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ahmed Breck Jezan, amesema kuwa
jumuiya hiyo imejikita katika kutoa huduma kwa watu wasiojiweza bila kujali
tofauti za kidini, kijinsia, kabila au rika.
"Majukumu yetu ni pamoja na
kusaidia yatima, wajane, wagonjwa na watu walioko katika mazingira hatarishi,
pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu na kuhamasisha jamii kuhusu
uadilifu,"
amesema Jezan.
Naye
Amili wa JAI Wilaya ya Kishapu, Said Hassan, amesema JAI pia inahamasisha
ushiriki wa jamii katika masuala ya afya, kuchangia damu, na kulinda mazingira
kama njia ya kukuza ustawi wa jamii.
Katika
risala iliyoandaliwa na uongozi wa JAI na kusomwa na Ustadh Abdallah Samiji,
taasisi hiyo imedhamiria kuendeleza mshikamano na amani, kuunganisha familia za
wagonjwa na kuwapatanisha watu waliokosana katika jamii.
Wakati
huo huo, viongozi mbalimbali walioshiriki hafla hiyo akiwemo Mwenyekiti wa
UVCCM Wilaya ya Shinyanga, Abdulaziz Said Sakala, wameipongeza JAI kwa kazi
nzuri na kuhimiza jamii kushirikiana na taasisi hiyo kwa ajili ya manufaa ya
pamoja.
Katibu
wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ashraph Majaliwa, amewashukuru waumini na wadau
waliounga mkono ujenzi huo na kushiriki hafla ya uzinduzi, huku akiishukuru
serikali na mashirika mengine kwa ushirikiano wanaoendelea kuupata.
Sheikh wa Mkoa wa
Shinyanga, Ismail Makusanya, akikata utepe ikiwa ni sehemu ya kuzindua Msikiti
mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata
ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.
Sheikh wa Mkoa wa
Shinyanga, Ismail Makusanya, akizungumza wakati wa kuzindua Msikiti mpya
unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata

Amili wa JAI Mkoa wa Shinyanga, Ahmed Breck Jezan, akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.
Amili wa JAI Mkoa wa
Shinyanga, Ahmed Breck Jezan, akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Msikiti
mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata
ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.
Amili wa JAI Wilaya ya Kishapu, Said Hassan, akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Ustadh Abdallah Samiji,
Amili wa JAI Wilaya ya Kishapu, Said Hassan, akisoma risala kwenye hafla ya kuzindua
Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika
mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Sheikh wa Mkoa wa
Shinyanga, Ismail Makusanya, akipokea risala iliyoandaliwa na JAI Mkoa wa
Shinyanga.

Waamini wakiwa kwenye hafla
ya kuzindua Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn, uliopo katika
mtaa wa Majengo Mapya, kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga leo Mei 9, 2025.

Katibu wa JAI Mkoa wa
Shinyanga, Ashraph Majaliwa, akiwashukuru waumini na wadau waliounga mkono
ujenzi huo na kushiriki hafla ya uzinduzi, huku akiishukuru serikali na
mashirika mengine kwa ushirikiano wanaoendelea kuupata.

Msikiti mpya unaoitwa Masjid Walidayn.
Post a Comment