" ZAIDI YA BILLION 15 ZIMEPATIKANA KUTOKANA NA MAUZO YA MADINI MKOANI SIMIYU.

ZAIDI YA BILLION 15 ZIMEPATIKANA KUTOKANA NA MAUZO YA MADINI MKOANI SIMIYU.


Na Neema Kandoro SIMIYU

ZAIDI ya bilioni 15 zimepatikana kutokana na mauzo ya madini Mkoani Simiyu katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Hayo yamebainishwa  wilayani Bariadi na Ofisa wa Madini Mkoani humo Mayigi Makolobela alipokuwa akizungumza na waandishi habari katika eneo hilo akielezea mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo.

Makobela alisema shilingi 15,280,993.09 zimepatikana katika kipindi hicho cha kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2025 kiasi ambacho ni kikubwa kuweza kufikiwa tangia kuanzia kwa ofisi hiyo Mkoani humo mwaka 2014.

Alisema leseni 573 za wachimbaji wadogo zimetolewa katika mkoa huo kutokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi yaliyowafanya wachimbaji hao kuwa na mwitikio wa kufanya shughuli hizo.

Makobela alisema kuwa kiasi hicho ni sawa na ongezeko la asilimia 300 ambayo ni mafanikio makubwa ukilinganikisha na miaka ya nyuma tangia kuanza kwa uchimbaji hapo mwaka 2014.

Aliendelea kutaja mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kutoa leseni tatu kwa vikundi vya wanawake (TAWOMA), kuanzisha vikundi vinne vya ununuzi wa madini, kupelekewa kwa baadhi ya maeneo umeme hivyo kuwapunguzia gharama za uendeshaji na kuwezeshwa kwa wachimbaji kuuza bidhaa hizo kwa bei kubwa.

Makobela alisema mafanikio mengine kuwa ni kuwezeshwa kwa wachimbaji wadogo kupata magari na mashine za kisasa za kucholonga hali ambayo imewafanya kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Aliongeza kusema kuwa tume ya madini Mkoani Simiyu inatoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha wachimbaji wadogo kuweza kumudu uendeshaji wa kazi zao za uchimbaji wa madini katika kipindi hiki cha sasa.

 Mmoja wa Wachimbaji mkoa wa Simiyu Bonaventure Makanga amempongeza waziri wa madini Anthony mavunde kwa kazi nzuri.anazofanya kwenye sekta hiyo nakumuomba amtembelee katika mgodi wake ili ampe ashauri wa namna ya kuendeaha kazi zake.



Post a Comment

Previous Post Next Post