Viongozi wa umoja wa wanawake wa Tanzania
U.W.T Wilaya ya Shinyanga Mjini wameanza ziara kwenye kata zote
kuimarisha uhai wa wanachama wake
Katika siku ya kwanza ya ziara yao,viongozi hao wa
U.W.T wamezungumza na wanachama wa jumuiya hiyo katika kata ya Ibadakuli
manispaa ya Shintanga ambapo wamehamasisha zaidi kuhusu uhai wa wanachama na
jumuiya zake, na kulipa ada kama inavyoelekezwa
Akizungumza katika mkutano uliojumuisha viongozi ngazi ya kata na matawii,pamoja na wenyeviti na wajumbe wa mitaa,vijiji na vitongoji wa kata hiyo, mwenyekiti wa U.W.T wilaya ya Shinyanga mjini Bi Rehema Nhamanilo amewataka kuendeleza umoja na mshikamano,kuwajibikia majukumu yao kwa weredi,ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya kikanuni, ili kukiimarisha chama na jumuiya zake
Mama Nhamanilo ameonya viongozi hao kuepuka makundi
yasiyokuwa na tija hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa
Rais,wabunge na madiwani,kwa kuwa yanaweza kusababisha mpasuko ndani ya chama.
Mwenyekiti huyo amesisitiza viongozi hao kuwa chachu
ya umoja na mshikamano zaidi miongoni mwao na kuepuka makundi
yasiyokuwa na tija.
Amewakumbusha kuendelea kuwapa ushirikiano wabunge na madiwani waliopo madarakani,ili kuwatia moyo waweze kukamilisha majuku yaliyo mbele yao.
kwa upande wake katibu wa U.W.T ( CCM) wilaya
ya Shinyanga mjini Getrude Mboyi amesisitiza zaidi kuhusu uhai wa jumuiya
hiyo na,ambapo amehamasisha kusimamia ulipaji wa ada,na kusajili
wanachama wapya.
Maadili,kupinga ukatili wa kijinsia, na wanawake
kujitokeza kwa wingi kugombea katika nafasi za uongozi ni kati ya mada
zilizowasilishwa na viongozi hao wa U.W.T wilaya ya Shinyanga mjini.
ziara hiyo iliyoanza Mei 12, 2025 inaendelea leo katika kata za Kizumbi na Ibinzamata.
MWISHO
mwenyekiti wa U.W.T wilaya ya Shinyanga mjini Bi Rehema Nhamanilo

Post a Comment