Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole na kueleza masikitiko yake kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea jioni Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba barabara kuu ya Moshi–Tanga Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro ambapo ajali hiyo imesababisha vifo vya Watu 37 na majeruhi 30 baada ya Magari mawili kugongana na kushika moto.
Kupitia ukurasa wake rasmi Rais Samia amewaombea marehemu wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka huku akitoa pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu pamoja na familia za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huo mkubwa.
Aidha Rais amesisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuwataka Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria hizo ili kupunguza ajali zinazogharimu maisha ya Watu wasio na hatia.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment