Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini,
Hussein Mohamed Bashe, amechukua fomu ya kuwania tena nafasi ya ubunge kupitia
Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza dhamira yake ya kuendelea kulitumikia jimbo
hilo endapo atapewa ridhaa tena.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu,
Bashe amewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na kusubiri utaratibu wa ndani
ya chama, huku akisisitiza kuwa iwapo jina lake litapitishwa, ataendelea
kusukuma gurudumu la maendeleo katika jimbo hilo.
"Niwaombe wananchi wa Nzega
Mjini waendelee kuwa wavumilivu wakati chama kikiendelea na mchakato wake wa
ndani. Tukiendelea kushikamana, tutaendelea kusukuma mbele gurudumu la
maendeleo kama tulivyofanya miaka yote," amesema Bashe.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment