Hali ya taharuki imetanda katika eneo la Mwatulole, Kata ya Buhalahala mkoani Geita, baada ya mtoto mchanga wa kiume anayedaiwa kuwa na siku mbili tu kupatikana ameuwawa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana, kisha kutupwa kwenye vichaka vilivyopo pembezoni mwa makazi ya watu.
Wananchi wameilalamikia hali hiyo na kuliomba Jeshi la
Polisi kufanya uchunguzi wa kina pamoja na kuwachukulia hatua wote waliohusika
na ukatili huo.
Viongozi wa mtaa huo pia wameomba vyombo vya dola
kuimarisha ulinzi na kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaojihusisha na
vitendo vya kukatisha uhai wa watoto ndani ya jamii.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Geita limefika
eneo la tukio na kuuchukua mwili wa mtoto huyo, huku uchunguzi wa awali ukianza
ili kubaini chanzo cha tukio hilo la kikatili.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment