Na Tonny Alphonce-Misalaba MediaShirika la Sense International Kwa kushirikiana na mashirika rafiki wamekabidhi choo Cha Wasichana na wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Mwaniko iliyopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza.Akielezea mradi uliofanikisha ujenzi huo,Mradi wa elimu shirikishi(DID-TO51) mratibu wa mradi wilaya Gerald Tuppa lengo ni kuondoa vikwazo vya ujifunzaji Kwa Wasichana na wanafunzi wenye ulemavu kusoma bila ubaguzi.Tuppa amesema hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa majengo mawili ya choo Kwa shule za Mwaniko na Mabuki majengo ambayo Yana matundu 6 yanayowawezesha watoto wenye mahitaji maalumu na chumba Cha kujistiri Kwa watoto wa kike.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa sherehe za kukabidhi choo hicho mwakilishi wa mkurugenzi wa Misungwi,Juliana Mwongerezi amesema maamuzi ya Sense International kusaidia ujenzi wa vyoo vya kisasa ulikuwa na uhitaji mkubwa hivyo umeleta mapinduzi makubwa ya elimu katika shule ya MwanikoJuliana amewataka Walimu na wanafunzi kuhakikisha wanakitunza choo hicho Kwa kukitumia vizuri Ili kiweze kusaidia na Watoto wengine watakaojiunga na shule hiyoNaye afisa maalumu wa wilaya ya Misungwi Charles Pamba amesema kilichofanywa na Sense International ni kile ambacho serikali imekuwa ikiomba kutoka katika mashirika Mbalimbali kusaidia katika maeneo ambayo serikali haijafanya.Pamba amesema ni kweli shule msingi Mwaniko ilikuwa na uhitaji wa darasa la watu wenye mahitaji maalumu pamoja na choo.Ujenzi wa choo na ukarabati wa darasa umetumia shilingi Milioni 20,311,760 ambapo ujenzi wa choo pekee ulitumia Milioni 11,340,214,gharama za ukarabati wa darasa na ofisi ya Mwalimu mkuu shilingi Milioni 5,586,664 ,gharama za ufundi Kwa shughuli zote Milioni 2,200,000, gharama za vifaa laki 338,538 na gharama za ufuatiliaji wa injinia wa wilaya laki 846,344



Post a Comment