" ALIYEWAHI KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA SHINYANGA, EMMANUEL NTOBI, AJIUNGA RASMI NA ACT WAZALENDO ATAJA SABABU

ALIYEWAHI KUWA MWENYEKITI WA CHADEMA SHINYANGA, EMMANUEL NTOBI, AJIUNGA RASMI NA ACT WAZALENDO ATAJA SABABU

 


 Na Mapuli Kitina Misalaba

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi, amethibitisha rasmi kujiunga na chama cha ACT Wazalendo katika mahojiano maalum na Misalaba Media.

 

Katika mahojiano hayo, Ntobi ameeleza kuwa uamuzi wake wa kuhamia ACT Wazalendo umetokana na kuvutiwa na sera za chama hicho na nia yake ya kuendelea kuhudumia wananchi kupitia jukwaa jipya la kisiasa.

 

Ntobi ameongeza kuwa amejiunga na ACT Wazalendo kwa sababu ya kuvutiwa na sera za chama hicho na nia yake ya kuendelea kuhudumia wananchi kupitia jukwaa jipya la kisiasa huku akisisitiza kuwa anatarajia kushirikiana na viongozi na wanachama wa ACT Wazalendo katika kuleta mabadiliko chanya nchini.

 

Uhamaji huu wa Ntobi unakuja wakati ambapo vyama vya upinzani nchini Tanzania vinaendelea kujiimarisha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. ACT Wazalendo, chini ya mwenyekiti, kimekuwa kikijitahidi kuvutia wanachama wapya na kuimarisha nafasi yake katika siasa za upinzani nchini.

 

Ntobi amesema kutokana na CHADEMA kukabiliwa  na changamoto za ndani, ikiwa ni pamoja na migogoro ya uongozi na mivutano kati ya viongozi wake wakuu ndiyo sababu ya  kuhamia chama kingine cha siasa.

Kwa sasa, bado haijafahamika ni nafasi gani Ntobi atapewa ndani ya ACT Wazalendo, lakini uamuzi wake wa kujiunga na chama hicho unaonekana kuwa ni hatua muhimu katika safari yake ya kisiasa.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post