Mwenyekiti wa bodi ya ligi Steven Mguto amethibitisha taarifa za kujiuzulu kwa aliyekua mjumbe wa kamati ya masaa 72 ndugu George Mayawa ambaye taarifa zake zilianza kutolewa tangu siku ya jana jumanne tarehe 3 Juni.
Mzee Mguto katika taarifa yake aliyoitoa siku ya leo Jumatano tarehe 4 Juni, ameeleza wazi kwamba ni kweli George Mayawa amendika barua ya kutaka kujiuzulu katika nafasi yake kutokana na sababu mbalimbali ambazo amezielekeza kwenye barua yake.
Mzee Mguto katika taarifa yake ameendelea kueleza kwamba George Mayawa katika barua yake ameainisha kwamba kwa sasa amekuwa na majukumu mengi sana kitu ambacho kinamfanya akose muda wa kutosha kuhudhuria vikao vya masaa 72.
Mguto pia amedokeza kwamba George Mayawa mara nyingi alikuwa anakosa muda wa kuhudhuria vikao kutokana na sababu kwamba amekuwa na majukumu mengine mengi ya kufanya na ndio maana amechagua kujiweka kando kwa wakati huu.
Mzee Mguto katika taarifa yake amemaliza kwa kusema kwamba kujiuzulu kwa George Mayawa hakuna uhusiano wowote na suala la mgomo wa klabu ya Yanga Sc kama inavyoelezwa na vyanzo mbalimbali vya habari za michezo nchini Tanzania.
George Mayawa ameamua kufanya maamuzi ya kujiuzulu kwenye nafasi yake kwa sababu hana nafasi ya kumudu ratiba ya vikao vya kamati hii na hilo linatokana na aina ya majukumu aliyokuwa nayo kwenye sekta zingine anazozisimamia, ameeleza Mzee Mguto.
Ni wazi kwamba George Mayawa hatakuwa sehemu ya kamati hiyo tena na pengine viongozi wanaweza kuangalia namna ya kuziba nafasi yakw kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo kwenye katika inayotumiwa na bodi katika kuendesha mambo yote ya ndani ya bodi ya ligi.
Post a Comment