" JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LAAHIDI KUMSAKA KWA NGUVU MUUAJI WA BERNARDO

JESHI LA POLISI MKOA WA SHINYANGA LAAHIDI KUMSAKA KWA NGUVU MUUAJI WA BERNARDO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi. Maria Raulent akizungumza kwa niaba ya familia ya marehemu.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Familia ya Daniel Masanja mkazi wa Tambukareli, Manispaa ya Shinyanga, imeliomba Jeshi la Polisi kuongeza juhudi katika kumtafuta mtuhumiwa anayedaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kijana wao, Bernardo Masanja, ili hatua za kisheria zichukuliwe na haki ipatikane.

Akizungumza kwa niaba ya familia hiyo, Maria Raulent amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Juni 22, 2025, ambapo marehemu Bernardo alikutwa amefariki dunia kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kifua akiwa eneo la karibu na kituo cha biashara ya bodaboda alikokuwa akifanya shughuli zake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Tambukareli, Bi. Tabitha Shilingi, amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kuwasilisha migogoro yao kwa viongozi wa serikali au taasisi za dini kwa ajili ya suluhu.

Akizungumza na Misalaba Media, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali dhidi ya mtuhumiwa.

“Kwanza napenda kuthibitisha kuwa tukio hili limeripotiwa rasmi ofisini kwangu tarehe 22 Juni 2025, majira ya saa sita usiku. Marehemu alifahamika kwa jina la Belenado Masanja, mwenye umri wa miaka 24, mkazi wa Tambukareli, ambaye alikutwa amechomwa kisu sehemu ya kifua upande wa kushoto,” amesema SACP Magomi.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa anayefahamika kwa jina moja la Kulwa alihusika katika ugomvi wa kugombea abiria na marehemu, ambapo wote wawili walikuwa waendesha bodaboda. Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kina na msako mkali unaendelea huku SACP Magomi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga na kwamba mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumanne wiki ijayo.

 



Post a Comment

Previous Post Next Post