" KAMENGE ANENA HAYA BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MISSENYI

KAMENGE ANENA HAYA BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MISSENYI


Evance Emmanuel Kamenge, mchumi na mkulima kutoka mkoani Kagera,amechukua fomu June 28,2025 ya kuwania ubunge katika Jimbo la Missenyi huku akiwatamanisha wana Missenyi kutokana na 
kauli zake zenye mvuto.

Akiongea na waadishi wa habari muda mfupi baada ya kuchukua fomu Kamenge amesema vipaumbele vyake muhimu bado vipo pale pale ikiwa ni kuangalia kuimarisha masuala ya kilimo na uchumi, ajira kwa vijana na kujenga mahusiano mazuri kimataifa.

"Nawashukuru sana wana Missenyi  siwezi kuwalipa kwa namna yoyote, ila nawaomba mniombee kwa Mwenyezi Mungu," alisema"Kamenge.

Amewataka wana Missenyi waendelee kumuunga mkono katika jitihada zake, huku akiahidi kuwa kama atafanikiwa kuwa mbunge, atakuwa mbunge wa vitendo kama alivyowaahidi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post