Kesi ya Tundu Lissu Yaahirishwa Ushahidi Haujakamilika
Mahakama imetoa amri kwa Jamhuri kuhakikisha wanakamilisha upelelezi kwani unapochukua muda mrefu ndivyo unavyoondoa haki ya mshtakiwa
Shauri limeahirishwa mpaka tarehe ijayo ikiwa ni kutokana na maelezo ya Jamhuri kusema wapo mwishoni katika kukamilisha upelelezi .
Ikumbukwe Baada ya hoja za Jamhuri kuwa Lissu ameidharau mahakama kwa kusema kauli No reform No election , Mawakili wa utetezi wakiongozwa na Mpale Mpoki, Dkt. Rugemeleza Nshala, Peter Kibatala na wengineo walipinga vikali na kuiomba Mahakama kufuta shauri hilo kwakuwa Jamhuri imeshindwa kukamilisha upelelezi kwa wakati, na kwamba kitendo cha kuchelewesha upelelezi ni kumnyima mtuhumiwa haki zake za msingi ikizingatiwa kuwa kupitia shauri hilo mtuhumiwa hawezi kujibu chochote
Kuhusu suala la mtuhumiwa kutoa maneno wakati anaingia Mahakamani, Mawakili wake wameileza Mahakama kuwa mtuhumiwa alicheleweshwa kuingizwa kwenye chumba cha Mahakama kwani ameingizwa kwenye chumba hicho sambamba na wakati Hakimu wa kesi husika anaingia, jambo ambalo limemkosesha mtuhumiwa uhuru wa kusalimiana na ndugu, jamaa na marafiki zake waliofika kumuunga mkono
Akitoa maamuzi, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Hakimu anayesikiliza shauri hilo amesema kwa mujibu wa sheria Mahakama inaanza tu pale Hakimu anapokuwa ameingia kwenye chumba cha Mahakama na kwamba kiutaratibu mtuhumiwa anapaswa kuingizwa kwenye chumba cha Mahakama baada ya Mahakama kuanza (yaani baada ya kesi husika kuitwa) na si vinginevyo, hivyo kutoa maelekezo kuwa utaratibu huo ndio unaopaswa kufuatwa hata itakapotajwa kwa wakati mwingine
Kuhusu suala la kutoa maneno wakati Mahakama imeanza, Hakimu amekubaliana na hoja za Jamhuri kuwa ni kweli mtuhumiwa ameidharau
Post a Comment