Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban Mwebea akizungumza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kata ya Ndala.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Diwani wa Kata ya Ndala ambaye pia ni Naibu
Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Zamda Shaban Mwebea, amewasilisha taarifa
ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 katika
kikao maalum na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Kata ya Ndala. Ambapo katika
utangulizi wake, amesema:
“Najiona mtu mwenye faraja, na mtu mwenye
upendo wa dhati kwa wananchi wenzangu wa Ndala. Aidha narudisha shukrani kwa
Mungu kwa hii miaka mitano hadi nafikia kusoma utekelezaji wa hii ilani, na
upendo wenu na maombi yenu ni faraja kwangu iliyonipa nguvu kusonga mbele na
kupambania maendeleo ya wana Ndala.”
Kata ya Ndala ni miongoni mwa kata 17 katika
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ikiwa na mitaa mitano: Banduka,
Mapinduzi, Mwabundu, Mlepa, na Ndala. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, ina
jumla ya wakazi 13,323; wanaume 6,359 na wanawake 6,964. Mtaa wa Mlepa
unaongoza kwa idadi kubwa ya watu huku Mapinduzi ukiwa na idadi ndogo zaidi.
Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ina kurasa
303, sura 10, na maneno 104,082. Kata ya Ndala imekuwa sehemu muhimu ya
utekelezaji wa ilani hiyo kwa vitendo.
ULINZI NA USALAMA
Kwa mujibu wa Ibara ya 105 (e) na (f) ukurasa
wa 157 wa ilani ya CCM, kata ya Ndala imeunda Kamati za Ulinzi na Usalama
katika ngazi ya kata na mitaa yote mitano. Taarifa zote za kiusalama zimekuwa
zikiwasilishwa na kufanyiwa kazi kwa wakati. Kwa zile zinazohitaji maamuzi ya
juu zaidi, zimekuwa zikiwasilishwa kwa mamlaka husika.
Zamda ameeleza kuwa kata hiyo imefanikiwa
kuimarisha ulinzi shirikishi kwa kuunganisha mitaa yote, kuviwezesha vikundi
vya sungusungu kwa vifaa vya usiku, na kupokea askari Polisi Kata aliye mratibu
wa shughuli zote za kiusalama. Polisi Kata huyo pia amekuwa mstari wa mbele
katika kuhamasisha uzalendo, uadilifu, na Polisi Jamii hasa kwa vijana na
wanafunzi.
HUDUMA ZA JAMII (MAJI, UMEME,
MAWASILIANO)
Kama ilivyoelezwa katika Sura ya 3 Ibara ya
77 ukurasa wa 124 wa ilani ya CCM, kata ya Ndala imepiga hatua kubwa katika
kuhakikisha huduma bora kwa wananchi wake.
Umeme
Mhe. Zamda amesema Mitaa yote mitano ya Ndala
imefikiwa na huduma ya umeme. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na:
·
Ufungaji wa
Transfoma mtaa wa Mapinduzi.
·
Ufungaji wa
Transfoma na nguzo mtaa wa Mlepa.
·
Usambazaji wa
nguzo na uunganishaji wa nyaya maeneo ya Ndala hasa eneo la Visiwani.
Miundombinu ya Barabara, Makalavati na
Madaraja
Kwa kipindi cha 2020-2025, jumla ya kilomita
5 za barabara zimechongwa katika mitaa ya Mwabundu, Mlepa na Ndala kwa ufadhili
wa Manispaa. Miradi mikubwa ni pamoja na:
·
Ujenzi wa
makalavati na mitaro mbalimbali.
·
Ujenzi wa Daraja
linalounganisha Ndala na Kambarage kwa gharama ya Tshs 103,252,840.
Jumla ya miradi ya barabara, makalavati na
madaraja imegharimu Tshs 440,725,740.
Mawasiliano
Amesema kata ya Ndala ina huduma nzuri ya
mawasiliano ya simu na intaneti katika mitaa yote mitano. Hii imesaidia
kuongeza kasi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Elimu
Kwa mujibu wa Sura ya 3 Ibara ya 79 ya ilani
ya CCM, kata ya Ndala diwani huyo amesema imepata mafanikio makubwa katika
sekta ya elimu.
·
Idadi ya
wanafunzi imeongezeka kwa 100% tangu 2021 hadi 2025 katika Shule ya Msingi
Msufini na Ndala Sekondari.
·
Ufaulu
umeongezeka hadi 98% mwaka 2024 katika Ndala Sekondari.
·
Motisha kwa
walimu na wanafunzi imeendelea kutolewa; walimu walipewa zawadi zenye thamani
ya TShs 180,000/=, wanafunzi walizawadiwa sabuni, madaftari na kalamu.
Miradi ya miundombinu ya elimu:
·
Ukamilishaji wa
chumba cha maabara ya sayansi: Tshs 30,000,000/= (2021).
·
Ujenzi wa vyumba
vya madarasa, matundu ya vyoo, madawati, viti na meza: Tshs 276,120,000/=.
Mhe. Zamda Shaban amewashukuru wananchi wote
wa kata ya Ndala kwa ushirikiano, upendo na maombi yao ambayo yamewezesha
mafanikio hayo huku akiahidi kuendelea kuwa kiongozi mwaminifu na mtumishi wa
watu hadi mwisho wa kipindi chake cha uongozi.
“Ndala ni yetu sote, maendeleo yake
yanatuhusu sote. Naendelea kuwahakikishia kuwa tutaendelea kushirikiana na
kuhakikisha ilani ya CCM inaendelea kutekelezwa kwa vitendo.”
ZAMDA SHABAN AWASHUKURU WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM KATA YA NDALA, "TUACHE SIASA ZA MAJITAKA"

Post a Comment