Rais Samia: Jeshi la Polisi Likomeshe Matukio ya Watu Kupotea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo ametoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuongeza umakini na kuchukua hatua madhubuti kukomesha matukio ya watu kupotea nchini.
Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, Rais Samia amesema kuwa kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuhusu matukio ya watu kupotea, hali inayozua hofu na kuathiri haki za binadamu.
“Nalitaka Jeshi la Polisi kuongeza umakini, kuchunguza kwa kina na kuhakikisha linakomesha kabisa matukio ya watu kupotea. Hili haliwezi kuvumiliwa katika nchi yetu yenye misingi ya haki, utu na usalama wa watu wote,” alisema Rais Samia huku akipigiwa makofi na wabunge.
Aidha, Rais Samia ameagiza vyombo vya usalama kwa ujumla kushirikiana na jamii kutoa elimu, kupokea taarifa na kuchukua hatua haraka dhidi ya vitendo vyote vinavyohatarisha usalama wa watu.
Rais pia amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuimarisha mifumo ya haki na ulinzi kwa kuhakikisha kila raia anapata ulinzi wa kutosha na anaishi kwa amani na uhuru ndani ya mipaka ya nchi.
Katika hotuba hiyo, Rais Samia pia amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na vyombo vya dola lakini akasisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya hasa kwenye ufuatiliaji wa matukio ya uhalifu yanayohusisha watu kupotea.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment