" SHIRIKA LA NELSAP LAWASOGEZEA HUDUMA YA MATIBABU WAKAZI WA RUSUMO KAGERA

SHIRIKA LA NELSAP LAWASOGEZEA HUDUMA YA MATIBABU WAKAZI WA RUSUMO KAGERA

Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Rusomo Dr Prisca Temba,akizungumza.

Na Mwandishi Wetu, Misalaba Media 

Wakazi wa Kijiji Cha Rusumo  kilichopo wilayani Ngara mpakani mwa Tanzania na Rwanda kimelishukuru Shirika la The Nile Equatorial  Lakes Subsidiary Action Program (NELSAP) Kwa kuwasogezea huduma ya afya.

Wakazi hao ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya katika hospitali ya wilaya wamesema kuanza kazi Kwa   kituo cha Afya Rusomo kimewapunguzia gharama na muda waliokuwa kufuata matibabu.

Rehema Musa mkazi wa Rusumo amesema kipindi Cha nyuma alipokuwa mjazito alilazimika kwenda mkoani Mwanza kwaajili ya kujifungua kutokana na kutokuwa na uhakika wa matibabu katika Kijiji hicho.

"Nilipokuwa nikiumwa nilikuwa napanda Pikipiki kwenda Mshikamano kwaajili ya matibabu,nimefurahi kupata kituo karibu na hapa nyumbani".alisema Rehema

Nae Damasi Justine amesema walikuwa wakipata changamoto kubwa hasa usiku ambapo walikuwa wakilazimika kukodi gari Kwa shilingi laki moja Ili kufika katika hospitali ya wilaya kwaajili ya matibabu.

Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo cha afya Rusomo Dr Prisca Temba amelishukuru Shirika la NELSAP Kwa kuwapatia vifaa tiba ambavyo vimeongeza ufanisi.

"Kwa Sasa tunatoa huduma zote Kwa wagonjwa wa nje na kulazwa pamoja na upasuaji na Kwa Sasa kituo kinapata idadi kubwa ya wagonjwa na wote wanahudumiwa".alisema Dr Temba

Mratibu wa NELSAP Dr.Eng Isack Alukwe  amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazonufaika na mradi wa Rusumo na hasa Kwa wakazi wa Ngara.

NELSAP imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali katika nchi za Africa zinazopitiwa na bonde la mto Nile Kwa Kushirikiana na serikali za nchi wanachama.
Mratibu wa NELSAP Dr.Eng Isack Alukwe, akizungumza.

Post a Comment

Previous Post Next Post