" Yanga Wasipocheza, Simba Bingwa 2024/25

Yanga Wasipocheza, Simba Bingwa 2024/25

 Eng Hersi

Eng Hersi

Yanga Wasipocheza, Simba Bingwa 24/25

Kufuatia Yanga kushikilia msimamo wa kutocheza mechi hiyo ya dabi, inaweza kuwa nafasi kubwa kwa Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
.
Yanga inabanwa na Kanuni ya 31 ya Ligi Kuu Bara Toleo la 2024 kifungu cha 1 (1.3) inayoelezea adhabu kwa timu itakayoshindwa kufika uwanjani itapokwa pointi 15.
.
Lakini mgomo huo wa Yanga kuna hatari kwao kupoteza nafasi ya pili itakayowapa tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao endapo itateleza katika mechi zilizobaki kisha Azam ikafanya vizuri.
.
Kanuni ya 31 ya Ligi Kuu Bara Toleo la 2024, kipengele (1) kinasema: “Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika kwa TFF/TPLB na/au kusababisha mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu zifuatazo: 1.1 Kutozwa faini ya shilingi milioni tano (5,000,000/-) ambapo shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000/-) itachukuliwa na Bodi ya Ligi Kuu na shilingi milioni mbili laki tano (2,500,000/-) italipwa kwa timu pinzani.
.
“1.2 Kulipa fidia ya maandalizi/uharibifu wowote unaoweza kujitokeza. 1.3 Kupokwa alama 15 (kumi na tano) katika msimamo wa Ligi na viongozi waliosababisha jambo hilo watachukuliwa hatua zaidi za kinidhamu. 1.3.1 Endapo timu itakuwa na alama pungufu ya 15, itakuwa na alama hasi kwa kiasi kinachopungua kwenye msimamo wa Ligi.
.
“1.3.2 Endapo timu itamaliza msimu wa Ligi ikiwa na alama hasi, itaanza na alama hizo hasi katika msimamo wa kwenye msimu unaofuata wa ya hadhi yake 14 Itapoteza haki ya kuchukua gawio lake la mapato ya mchezo huo.
.
“1.5 Kiongozi yeyote atakayebainika kushiriki, alishawishi au alikuwa chanzo au sababu ya timu kutotokea uwanjani bila ya sababu za msingi atafungiwa kwa kipindi cha miezi kumi na miwili (12).”

Post a Comment

Previous Post Next Post