Chadema Kwenda Mahakamani Kupinga Uamuzi wa Msajili
Kamati Kuu ya CHADEMA baada ya tafakari ya kina imeamua kwenda Mahakamani ikisema imeshindwa kuiona nia njema ya Msajili wa Vyama vya siasa katika maamuzi yake aliyoelekeza kwenye barua aliyowapa CHADEMA na taarifa yake kwa umma.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara John Heche Kamati Kuu, imewaelekeza Wanasheria wa chama kuwa hadi kufika Alhamisi June 19,, 2025, shauri hili liwe limepelekwa Mahamamani.
“Madai yeyu ya msingi ni kwa kwa sababu tumejiridhisha kuwa Msajili wa Vyama vya siasa hana mamlaka kutafsiri Katiba ya Chama kwa namna anavyoona yeye tofauti na uhalisia wenyewe, hii inatokana na Msajili kwa msukumo wake mwenyewe kutoa tafsiri kuhusu uchaguzi na tukio la uthibitisho wa walioteuliwa na kutakiwa kufanyika uamuzi wa kuwathibitisha kwenye kikao cha baraza kuu”
“Sababu aliyoitoa msajili wa vyama vya siasa ya kuzuia ruzuku ya kila mwezi kwa CHADEMA imepotoka na kwenda kinyume na sheria ya vyama vya siasa ibara 18 (6), ambayo inaeleza kuwa ruzuku itasitishwa endapo bodi ya wadhamini ya chama haina uwezo wa kusimamia fedha za chama, kitu ambacho sio sahihi. Bodi ya wadhamini ya CHADEMA ipo chini ya Uenyekiti wa Mama Ruth”
“Msajili hana mamlaka ya kubatilisha maamuzi halali ya vikao vya chama kwa mujibu wa Katiba ya Chama na pia Msajili wa Vyama vya siasa sio mamlaka ya rufaa na sio chombo cha kupokea malalamiko yoyote kwa masuala ya Chama na Wanachama wa Chama cha siasa”
Post a Comment