" TRUMP AWATISHA WASHIRIKA WA PUTIN

TRUMP AWATISHA WASHIRIKA WA PUTIN


Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media

Rais  wa marekani  Donald  Trump ametoa kauli kauli ya kitisho cha vikwazo kwa washirika wa Urusi. 

Aliyasema hayo Leo  alipomkaribisha katika Ikulu ya White House ya nchin  Marekani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Mark Rutte ambaye ameipokea taarifa hiyo kwa bashasha na kusema kwamba hiyo ni habari kubwa na muhimu kwa Waukraine.

Itakumbukwa kwamba Rais Trump aliahidi kuvimaliza vita ya Ukraine ndani ya muda wa saa 24 ikiwa angechaguliwa kwa muhula wa pili kama rais wa Marekani lakini mpaka sasa tangu arejee kwenye kiti hicho juhudi zake bado hazijazaa matunda.

Hayo yanajiri saa chache baada ya mjumbe maalum wa Marekani Keith Kellog kuitembelea Ukraine na kutoa mwito kwa Urusi kusitisha vita mara moja na kuingia kwenye mazungumzo ya pande tatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post