Klabu ya Azam Fc imemtambulisha aliyekuwa kocha wa Al
Hilal ya Sudan, Florent Ibenge kama kocha wao mkuu klabuni hapo akichukua
mikoba ya Rachid Taoussi aliyeoneshwa mlango wa kutokea baada ya kutamatika kwa
msimu uliopita.
“Kama ligi ya Tanzania ni namba nne kwa ubora basi timu zilizopo zina ushindani mkubwa lakini anaamini amekuja kupamba ili aweze kufikia mafanikio na wao wapo kwenye nafasi ya ushindani,” alisema na kuongeza.
“Simba msimu huu imecheza fainali ya Kombe la Shirikisho ni namna gani kuna timu bora lakini pia kuna Yanga ambayo imetwaa mataji yote msimu huu nahitaji ushindani mkubwa kutoka kwao nipo tayari kwa ushindani.”
Ibenge amesema anatambua ana cv kubwa lakini hiyo haitoshi kuipa mataji Azam
bila kuwekeza nguvu kwenye kujenga timu bora kilichomleta Tanzania ni kuipambania
timu hiyo kutwaa mataji ndani na kimataifa.
Post a Comment