" CHADEMA Waendelea Kumkataa Jaji Mwanga, Kesi Yaahirishwa

CHADEMA Waendelea Kumkataa Jaji Mwanga, Kesi Yaahirishwa

 

Kesi namba 8323/2025 ya mgawanyo wa rasilimali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyokuwa inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 14, Julai 2025 saa nne asubuhi.

Ahirisho hili limekuja baada ya mawakili wa upande wa waleta maombi kuiomba mahakama kupata muda wa kwenda kuisoma na kutafakari barua iliyopelekwa mahakamani hapo na upande wa wajibu maombi (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu).

Wakili wa wajibu maombi Mpale Mpoki aliieleza Mahakama kuwa wateja wake waliandika barua kwenda kwa Naibu Msajili wa Mahakama kuomba na kutaka Jaji Hamidu Mwanga ajitoe kusikiliza kesi namba 8323/2025.

Wakili Mpoki ameileza mahakama kuwa walichelewa kuupatia upande wa waleta maombo nakala ya barua kutokana na kwamba barua hiyo ilikuwa ni ya mahakama tu hivyo hawakufahamu kama upande wa waleta maombi wanapaswa kuapatiwa nakala ngumu.

Hata hivyo kuahirishwa kwa shauri hilo kunaathiri maombi yaliyowasilishwa mahakamani na upande wa CHADEMA ya kuiomba mahakama kufuta uamuzi alioutoa Jaji Mwanga Juni 10, juu ya kusimamishwa kwa shughuli za CHADEMA.

Post a Comment

Previous Post Next Post