Na Tonny Alphonce, Misalaba Media
Katika kuadhimisha Siku ya Kuzuia Kuzama Maji Duniani, Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo EMEDO limezindua rasimi Sheria ndogo za Uvuvi zenye lengo la kuimarisha usimamizi wa shughuli za uvuvi na kuongeza usalama wa wavuvi katika maji.
Akizungumza katika maadhisho hayo ya Kuzuia Kuzama Maji Duniani yaliyofanyika kisiwa cha Mulumo, kilichopo Mazinga, Wilaya ya Muleba mgeni rasimi Mwanasheria wa Wilaya Mr Muyengi Muyengi amesema Sheria hizo zilizopitishwa ni vizuri zikafuatwa kwakuwa wale wote watakaovunja Sheria hizo watapewa adhabu ikiwemo faini kwa baadhi ya makosa.
"Uzuri Sheria hizi mlishirikishwa wakati zinatengenezwa na Sasa mnajua ukikamatwa hujavaa Jacket la Uokozi adhabu yake ni nini"alisema Muyengi.
Nae fisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka EMEDO Leonard Masele amesema maadhimisho hayo mbali na kuzindua rasimi Sheria hizo ndogo za uvuvi lakini pia wametoa elimu ya usalama majini Ili kuongeza uelewa kuhusu matumizi ya vifaa vya kujiokoa, na kuhimiza tabia ya kuwajibika wakati wa shughuli za uvuvi.
Nae mkuu wa kituo Cha Polisi kata ya Mazinga OCS Nathani Mwakyusa amewataka wamiliki wa mitumbwi kuzingatia pia Suala la usafi na uhifadhi mzuri wa Makoti ya Uokozi Ili Kila mmoja aweze kutumia bila kulazimishwa.
Post a Comment