Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Faisal D. Lujiga, amerudisha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake ili kuwania nafasi ya Udiwani katika Kata ya Maganzo, Halmashauri ya Mji wa Kishapu mkoani Shinyanga.
Lujiga amerudisha fomu hiyo leo Julai 1, 2025 katika ofisi ya katibu wa CCM Kata ya Maganzo, ikiwa ni ishara ya kukamilisha hatua muhimu ya kuomba uteuzi ndani ya chama hicho tawala kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Faisal amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira yake ya dhati ya kulitumikia taifa kupitia nafasi ya uongozi wa kata, akiahidi kushirikiana na wananchi wote katika kusukuma mbele maendeleo ya Maganzo.
Zoezi la urejeshaji wa fomu kwa wagombea ndani ya CCM linaendelea kote nchini huku chama hicho kikisisitiza misingi ya demokrasia, uwazi na ushindani wa haki katika mchakato mzima wa kupata viongozi bora.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment