" GLOBAL EDUCATION LINK LTD YAWAAHIDI WATANZANIA UHAKIKA WA ELIMU

GLOBAL EDUCATION LINK LTD YAWAAHIDI WATANZANIA UHAKIKA WA ELIMU

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Global Education Link, Abdulmalik Mollel

 

Na, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha. 

Wanafunzi  wamejitokeza kwa kishindo na kuhakikishiwa namna ya kupata elimu bora na ya uhakika katika mataifa mbalilbali duniani kupitia   Global Education Link Ltd. 

Akizungumza na Wanahabari katika maonyesho ya vyuo vikuu duniani Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Education Link  ltd Abdulmalik Mollel amesema ni wakati muafaka kwa watu wote wanaohitaji kujiendeleza kielimu katika vyuo vikuu   Duniani ili kukuza wao na Taifa kwa ujumla. 

Aidha amesema kuwa Kwa Kanda ya Kaskazini mwitikio wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya nje umekuwa mkubwa, hatua inayoonyesha kuwa uhitaji wa elimu nchini ni  mkubwa.

"Hatua hii kwetu imetupa chachu ya kuwasogezea watanzania wote mwanga huu, wazazi na watoto wao wana imani na taasisi hii, nasi tunaahidi kuwahudumia na kuhakikisha wanapata elimu bora kama wanavyotaka", 

" Mpango wetu ni kuzifikia kanda zote nchini, na baada ya hapa tutakuwa Kahama lengo ni kuwapa mwanga watu wote wanaotaka kusoma vyuo vya nje ya nchi wajue wanaanzia wapi na vyuo gani bora wanavitaka, gharama ni nafuu na kila mwenye nia atasoma" amesema Mollel. 

Mmoja wa wanufaika wa  maonyesho hayo Daniel Kaaya amesema taasisi ya Global imempa mwanga na uhakika wa asilimia mia kusoma nchini India katika chuo kikuu cha RSM elimu ya uzamivu (Masters). 

Wazazi na watoto wao waliojitokeza kutafuta nafasi za masomo nje ya nchi kwenye maonyesho ya Global Education Link Ltd

"Mimi ni mtumishi wa serikali na nimekuwa nikitamani kuongeza elimu ya uzamivu muda mrefu, nashukuru sana taasisi ya Global imenihakikishia nitasoma bure kwa upande wa ada, ninachotakiwa kutafuta ni pesa ya nauli, malazi na chakula, kwa sasa ninaanza kujipanga ili muda wowote nianze safari kuelekea nchini India"amesema.

Katika namna hiyohiyo Nancy Mollel amepata nafasi katika chuo kikuu cha MMU nchini India, kwenda kusoma kozi ya uhasibu ngazi ya stashahada, ametoa wito kwa wananfunzi wote wanahitaji kujiendeleza katika vyuo vya nje kuwasiliana na Global Education Link Ltd. 

"Nina furaha sana, naona ndoto zangu zinaenda kutimia, nawashukuru sana taasisi ya Global kuja Arusha, napendekeza wafike kila mkoa maana wenye uhitaji ni wengi na hawajui pa kuanzia" amesisitiza Nancy.

Post a Comment

Previous Post Next Post