" SHANGWE ZATAWALA MAKABIDHIANO YA MAENEO YA UJENZI WA SOKO KUU NA STENDI MPYA MANISPAA YA BUKOBA

SHANGWE ZATAWALA MAKABIDHIANO YA MAENEO YA UJENZI WA SOKO KUU NA STENDI MPYA MANISPAA YA BUKOBA

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media – Bukoba

Leo ni shangwe kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Kagera hususan wa manispaa ya Bukoba  wanaoenda kushuhudia hatua za miradi mikubwa ya maendeleo katika Jimbo la Bukoba mjini chini ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dokta. Samia Suluhu Hassan

Miradi mikubwa iliyosubiriwa kwa hamu kubwa ni pamoja na ujenzi wa soko kuu jipya la Manispaa ya Bukoba, ujenzi wa stend mpya ya Kyakailabwa, ujenzi wakingo za mto kanoni,uwekaji wa taa za barabarani na ujenzi wa barabara zaidi ya kilomita kumi.

Hata hivyo hafla hiyo inafanyika eneo la soko kuu Bukoba huku mgeni akitarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Kagera mhe, Hajjat Fatma Mwassa.

Makundi mbali mbali ya ngoma kutoka Manispaa ya Bukoba, Ngara na msanii wa Kagera Shemela wamepamba hafla hiyo kwa ngoma na burudani mbali mbali wakionyesha furaha kubwa ya kushuhudia miradi hiyo mikubwa ambayo inakwenda kuwa hatua ya kukuza mji wa Bukoba ikiwa ni awamu ya pili (TACTICS TIER2) ZONE 3

Miradi hii inatarajiwa kubadili kabisa taswira ya mji wa Bukoba, kukuza uchumi wa maeneo ya mijini, na kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera.






 

Post a Comment

Previous Post Next Post