JOHN STEPHANO LUHENDE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA BUKENE – NZEGA
Officialgamaya0
Na. Elias Gamaya Nzega Tabora
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Shirika
la Luhende John Foundation lenye makao yake makuu Wilaya ya Nzega,
mkoani Tabora, Ndg. John Stephano Luhende amechukua fomu ya kuomba
ridhaa ya kugombea ubunge wa Jimbo la Bukene kupitia CCM.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Ndg. Luhende amesema
kuwa uamuzi wake umetokana na nia ya dhati ya kuleta mabadiliko chanya katika
jimbo hilo, kwa kushirikiana na wananchi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
“Nimeshawishika kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kwa
wananchi wa Bukene ili tufanye mabadiliko na kuharakisha maendeleo ya kijamii
na kiuchumi. Nina imani kuwa kwa kushirikiana na wananchi, tunaweza kulijenga
upya jimbo letu,” amesema Ndg. Luhende.
Post a Comment