HomeHABARI KADA CHADEMA ABWAGA MANYANGA ATUA CCM... ASEMA KAFURAHISHWA NA KAZI NZURI ZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN Misalaba July 02, 2025 0 Na Gift Mongi, MoshiAliyekuwa kada wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)na diwani wa kata ya Kiboriloni kwà mwaka 2020-2025 Frank Kagoma amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM).Kagoma amepokelewa hii leo julai 2.2025 na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Moshi mjini Faraji Swai katibu wa chama hicho Frida Kaaya na mbunge wa jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo sambamba na wajumbe wa kamati ya siasaPamoja na kukihama chama hicho Kagoma amechukua fomu ya uteuzi ndani ya chama hicho kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya udiwani.Alisema alitafakari kwa kina na kuona maendeleo yaliyofanywa na rais Dkt Samia Suluhu HASSAN hivyo ameona ni vyema kuungana naye katika kuleta maendeleo kwa wananchi kwa hivi sasa."Nilikuwa katika safari ya kuelekea Dar es Salaam hivyo kufika Wami injini ikadondoka nikaona ni bora nipande gari lingine'alisemaKagoma ambaye katika baraza la madiwani lililomalizika alikuwa ni diwani pekee kutoka chama cha upinzani(CHADEMA)amesema baada ya kufuatwa na wazee amehamua kufanya maamuzi hayoKwa upande wake Faraj Swai amesema kuwa amefanya maamuzi sahihi na kuwa kwa kipindi cha miaka mitano amekuwa akitekeleza ilani ya chama cha mapinduzi hivyo ni vyema sasa akitumikia moja kwa mojaFrida Kaaya ambaye ni karibu wa CCM wilaya ya Moshi Mjini alisema kuwa chama hicho kipo tayari kumpa mwanachama huyo ushirikiano kwa namna yoyote ile lengo likiwa ni kuleta maendeleo kama ambavyo ni dira ya chama hicho.Mara baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha mapinduzi Kagoma akiongozwa kiapo cha chama hicho kilichosemwa na karibu wa uenezi itikadi na mafunzo wilaya ya Moshi Mjini Athuman Ally.Mwisho 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment