" NEST YATATUA MWAROBAINI WA RUSHWA

NEST YATATUA MWAROBAINI WA RUSHWA

VIJANA wanaojishughulisha na shughuli za uzalishaji mali wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuanzisha mfumo wa manunuzi wa nest kwani imerahisisha na imeweka uwazi masuala ya upatikanaji wa tenda kutoka kwenye Taasisi za Umma.Wakizungumza  6/7/2025 jijini Mwanza vijana hao walisema Mfumo wa ununuzi kwa njia ya mtandao unapunguza haja ya kuwasiliana ana kwa ana na wazabuni na taasisi zinazohitaji huduma, pia utasaidia kuhakikisha ushiriki sawa na mpana wa Wazabuni na hivyo kupunguza mianya ya rushwa. Walisema mfumo huu ni wa uwazi kwa kuwa kila mchakato wa manunuzi ya Umma unaofanyika ndani ya mfumo, kila aliyepewa dhamana ya kuingia kwenye mfumo huo atakuwa anaona au kujua kinachoendelea humo hivyo kupunguza changamoto ya rushwa wakati wa mchakato wa kutangaza zabuni.Mnufaika wa mfumo huo Enock Bigaye Mwenyeji wa Nyamagana Jijini la Mwanza mwenye Kampuni ya Begas ambaye anasambaza vifaa vya maabara na vya ujenzi wa miundombinu mashuleni aliipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo huo kwani inamurahisishia upatikanaji wa tenda huku malipo ya kazi zake akisema anapata baada ya siku mbili hadi tatu akimaliza kazi.Alisema amekuwa akipata tenda mbalimbali za kusambaza vifaa vya maabara kwenye shule mbalimbali hapa nchini kwani amekuwa akitoa huduma hizo kwa bei rafiki hivyo kuvutia wadau hivyo kujipatia tenda nyingi."Unachotakiwa ni kutokuweka bei kubwa ya utoaji wa huduma hali hiyo inavutia taasisi na vilevile ubora wa vifaa vyako ni mhimu uzingatie"alisema Bigaye.Bigaye aliwataka vijana wenzake wajisajiri kwa ajili ya kutumia mfumo wa Nest kwani imeonesha mafanikio makubwa katika ufanyaji kazi wa kila siku huku ukirahisisha namna ya upatikanaji wa malipo ya tenda wanazopata.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA 

Post a Comment

Previous Post Next Post