Mwanaharakati kijana na mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nuru Mwalembe Kaitwike, ameonyesha dhamira yake ya dhati ya kulitumikia taifa kwa kuchukua na kurudisha fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani Viti Maalum katika Kata ya Pangani.
Hatua hiyo imefanyika kwa utulivu na nidhamu, ikionyesha uzito na heshima aliyonayo kwa nafasi hiyo ya uongozi. Nuru, ambaye ni miongoni mwa wanawake wanaochipukia kisiasa, amesema:
“Nimeamua kuchukua na kurudisha fomu kwa moyo wa upendo kwa jamii yangu na chama changu. Ninaamini wanawake wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo ya kweli katika jamii zetu.”
Tukio hilo limepokelewa kwa shangwe na wanachama pamoja na wakazi wa Pangani waliompongeza kwa ujasiri wake na uzalendo. Kwa sasa, safari ya kuelekea mchakato wa kura za maoni ndani ya chama inaendelea, huku wajumbe wa UWT katika kata hiyo wakitarajiwa kushiriki kikamilifu.
Post a Comment