Bwana Richard Jared Mpongo ni miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliowasilisha fomu za kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Kizumbi, Jimbo la Shinyanga Mjini.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Richard alisema kuwa ameamua kutumia haki yake ya kikatiba ya kugombea nafasi ya kuchaguliwa kama Mtanzania, akilenga kuchangia maendeleo ya jamii.
Ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Kizumbi kumuunga mkono katika safari ya kuleta maendeleo endelevu, akiahidi kushirikiana nao kikamilifu endapo atapewa nafasi hiyo.
Aidha, alibainisha kuwa kupitia kikao cha kitaifa cha watu wenye ulemavu, wamehamasishana kushiriki kikamilifu katika uongozi, akisisitiza kuwa watu wenye ulemavu wana uwezo na haki sawa na wengine katika kushiriki nafasi mbalimbali za uongozi nchini.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment