" UBIA WA BARRICK NA TWIGA WAPAISHA UCHUMI WA TANZANIA

UBIA WA BARRICK NA TWIGA WAPAISHA UCHUMI WA TANZANIA


Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Julai 7,2025 katika Mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Na. Edwin Soko
Kahama, Shinyanga

Ubia wa  Kampuni Barrick  na Twiga  katika sekta ya Madini  i umezidi kuongeza thamani ya pamoja na kuinua uchumi wa Tanzania.

Hayo yamebainishwa na   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Mark  Bristow alipokuwa anaongea na waandishi wa Habari kwenye mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Julai 7, 2025 Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

" Tulipoanzisha Twiga , lengo lilikuwa zaidi ya kusuluhisha  changamoto za kihistoria na   kujenga mustakabali mpya kwa kufungua utajiri wa Dhahabu wa Tanzania  kwa njia inayogawanywa kwa haki manufaa yake na kujenga thamani ya kudumu  kwa wadau wote. Baada ya miaka mitano tumeirejesha Barrick katika hali ya kuwa na mchango mkubwa kwenye uchumi wa Nchi" Alisema Bristow.

Pia alisisitiza kuwa, Tangu Barrick ichukue rasmi uendeshaji wa migodi mbalimbali hapa Nchini mnamo Mwaka 2019, Kampuni hiyo imeingiza dola bilioni 4.79 katika Uchumi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na Dola Milioni 558 katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2025.

Bristow alibainisha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya ununuzi wa  huduma umeendelea kufanyika kutoka  kampuni za kitanzania , ambapo nyingi kati ya hizo ni za wazawa, huku asilimia 95 ya wafanyakazi wake wakiwa watanzania na asilimia  49 walitoka katika jamii zinazozunguka migodi.

Bristow alisisitiza kuwa, ubia na Twiga haukusaidia tu  kurejesha utulivu na uendeshaji wa migodi bali pia imejenga msingi wa ushawishi wa thamani ya muda mrefu kupitia umiliki wa pamoja  uwezeshaji wa wenyeji na mkabala wa kiuwajibikaji na kuleta maendeleo.

Naye Meneja wa Nchi, Tanzaniawlkiory Ngido alisema kuwa, Barrick imekuwa na utaratibu wa kutoa taarifa ya Kila robo Mwaka kwa Vyombo vya habari na wadau wa sekta ya madini hapa Nchini inafanya hivyo ili kutoa taarifa sahihi Kwa watanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post