" Waliokufa Ajali ya Same Wafikia 42

Waliokufa Ajali ya Same Wafikia 42

 


Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya barabarani, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, imeongezeka na kufikia 42.

Wakati idadi hiyo ikiongezeka, serikali ikitangaza kuwa uchunguzi wa awali majibu ya vipimo vya sampuli za vinasaba (DNA), vimeonyesha mafanikio makubwa katika uchunguzi wa vinasaba vya ndugu.

Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu, akitoa leo Julai 02, 2025, utaratibu wa mazishi kwa wahanga wa ajali hiyo, amewataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kesho, Julai 3, 2025 katika Hospitali ya Rufani ya Kanda ya KCMC kuaga miili hiyo.

“Nimshukuru pia mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kugharamia matibabu yote kwa majeruhi wote, kuelekeza utaratibu wa zoezi la mazishi ya miili 36 iliyobaki pamoja na kutoa mkono wa pole kwa familia 42 zilizopoteza wapendwa wao,”amesema Babu.

Ajali hiyo iliyotokea Juni 28, 2025 katika la Sabasaba, Kitongoji Mahuu, Kata ya Same, takribani kilomita nne kutoka Same mjini, ililibusisha basi kubwa la abiria, mali ya Kampuni ya Chanel One, namba T 179 CWL na basi dogo la abiria aina ya Coaster, T 199 EFX linalomilikiwa na Kampuni ya Mwami Trans.

Coaster hiyo ilikuwa ikitokea Same kuelekea Manispaa ya Moshi, wakati basi la Chanel One lilikuwa likitokea Arusha kuelekea Tanga.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post