CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani kimetangaza majina ya wagombea Udiwani 136 watakaokiwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Mjini Kibaha Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Pwani David Mramba alisema kuwa madiwani hao ni wale walioongoza kwenye kura za maoni.
Alisema kuwa walioshinda siyo kwamba ni bora sana bali nafasi ilikuwa ni moja tu hivyo wawakilishe vyema chama kwenye uchaguzi mkuu.
Mkoa una jumla ya Kata 136 hivyo kufanya madiwani 163, Viti MaalumTarafa ni madiwani 27, na wagombea kupitia kapu ni wawili hivyo kufanya Madiwani wa mkoa huo kuwa 165.
Aidha alisema kuwa majina hayo yamerudishwa kutoka CCM Makao Makuu baada ya uchaguzi wa kura za maoni zilizofanyika kote nchini.
Post a Comment