" CCM YAWEKA RATIBA YA KAMPENI KOLANDOTO, KICKOFF AGOSTI 28, CDE MOSES MSHAGATILA ATAMBULISHA FALSAFA YA "KOLANDOTO YETU, KESHO YETU"

CCM YAWEKA RATIBA YA KAMPENI KOLANDOTO, KICKOFF AGOSTI 28, CDE MOSES MSHAGATILA ATAMBULISHA FALSAFA YA "KOLANDOTO YETU, KESHO YETU"

CDE MSHAGATILA ACHUKUA FOMU KUWANIA UTEUZI UDIWANI KATA YA KOLANDOTO 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mgombea udiwani kata ya Kolandoto kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Moses Mshagatila, ametangaza falsafa yake ya kuongoza wananchi wa kata hiyo mara baada ya kuchukua fomu ya uteuzi, akisema dira yake ni “Kolandoto yetu, Kesho yetu.”

Mshagatila anasema falsafa hiyo ndiyo itakayojenga mshikamano wa wananchi wa Kolandoto kwa umoja na upendo, akisisitiza kuwa hakuna mtu mwingine atakayeijenga kata hiyo isipokuwa wenyewe.

Aidha, amesema chama chake cha CCM kipo imara chini ya mwenyekiti wa taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akibainisha kuwa utekelezaji wa ilani ya chama umeendelea kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mshagatila amewahakikishia wanachama na wananchi wa Kolandoto kuwa hatakuwa kiongozi wa ofisini pekee, bali atakuwa karibu nao katika changamoto na furaha zao, huku akiahidi kusimamia haki, kuunganisha wananchi na kuwa msikivu wa mahitaji yao.

Ameeleza kuwa changamoto na mahitaji ya Kolandoto anayafahamu vyema, na akaongeza kuwa hatakubali kuyumbishwa na mtu ama kikundi chochote, badala yake atasimama kidete kutekeleza maagizo na maelekezo ya chama chake.

Vilevile, amewataka wanachama wa vyama vingine vya siasa kuchukua fomu na kujiandaa kwa mapambano ya kisiasa tarehe 28 Agosti 2025, ambapo kampeni rasmi zinatarajiwa kuanza katika kata hiyo.

Kwa mujibu wa katibu wa CCM kata ya Kolandoto, maandalizi ya kampeni za kumtambulisha na kumnadi mgombea wao katika kata ya Kolandoto yamekamilika tayari ambapo tarehe 28 Agosti kampeni zitaanza.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kolandoto kupitia CCM, Moses Mshagatila, akikabidhiwa fomu ya uteuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Kolandoto kupitia CCM, Moses Mshagatila, akikabidhiwa fomu ya uteuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post