Na Mwandishi wetu, Misalaba Media
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kimetangaza matokeo ya kura za maoni za ubunge kwa Jimbo la Geita Mjini, ambapo Chacha Mwita Wambura ameibuka kinara kwa kupata kura 2,145.
Akifuatia kwa karibu ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Constantine Kanyasu, aliyepata kura 2,097.
Akitangaza matokeo hayo leo, Katibu wa CCM Wilaya ya Geita, Michael Msuya, amesema wagombea wengine walioshiriki mchakato huo ni John Lugola Saulo aliyepata kura 39, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi kura 119, na Upendo Furaha Peneza aliyepata kura 1,272.
Kwa mujibu wa Katibu huyo, jumla ya wajumbe waliojiandikisha walikuwa 6,588 huku 5,726 wakijitokeza kupiga kura. Kura zilizoharibika zilikuwa 57 na kura halali zilikuwa 5,682.
Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM ni sehemu ya maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Post a Comment