" CHIFU ANTONIA SANGALALI ATOA MILIONI MOJA KUSAIDIA KAMPENI ZA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN

CHIFU ANTONIA SANGALALI ATOA MILIONI MOJA KUSAIDIA KAMPENI ZA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN

Mwenyekiti wa Machifu Tanzania na Ntemi wa Himaya ya Jigoku (Masela) Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Chifu Antonia Sangalali, ametoa mchango wa Shilingi 1,000,000/= (Milioni moja) kwa ajili ya kumsaidia Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuendesha kampeni zake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Chifu Sangalali amesema mchango huo ni sehemu ya kuonyesha mshikamano na kumuunga mkono Rais Samia kutokana na kazi kubwa ya maendeleo aliyofanikisha katika kipindi cha uongozi wake.

“Natoa mchango huu wa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kumpa nguvu Mama Samia Suluhu Hassan katika kampeni zake. Amefanya mengi kwa taifa hili na anapaswa kuungwa mkono ili aendelee kutekeleza miradi ya maendeleo,” amesema Chifu Sangalali.

Ameeleza kuwa viongozi wa kimila wana nafasi kubwa katika kushirikiana na viongozi wa kisiasa kuhakikisha taifa linaendelea kudumisha amani, mshikamano na maendeleo endelevu.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post