" KYOMBO APANIA KUKILETEA USHINDI MNONO CHAMA CHA MAPINDUZI KAGERA

KYOMBO APANIA KUKILETEA USHINDI MNONO CHAMA CHA MAPINDUZI KAGERA

Na Lydia Lugakila 

Missenyi 

Mgombea ubunge wa Jimbo la Missenyi Mkoani Kagera kupitia chama cha mapinduzi (CCM) amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za tume huru ya uchaguzi wilayani humo, huku akiahidi kushirikiana kwa karibu na wanachama wenzake pamoja na wananchi wote ili kuhakikisha chama chake kinashinda na kuendelea kushika dola.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Florent Laurent Kyombo alisema ana nia ya dhati ya kulijenga Jimbo la Missenyi kwa kutekeleza ilani ya chama chake na kusimamia vipaumbele vya wananchi, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, elimu, maji safi, barabara na kilimo.

“Ninajua kuwa maendeleo hayawezi kufanikishwa na mtu mmoja, ndiyo maana nawaomba wanachama wenzangu, viongozi wa chama na wananchi wote tushikamane kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya watu wetu inatekelezwa kikamilifu,” Kyombo.

Amesema kuwa atatumia uzoefu wake Bungeni na uhusiano wake na serikali kuhakikisha miradi iliyoanzishwa inakamilika na mipya inaanzishwa kulingana na mahitaji ya wananchi wa Missenyi.

Wananchi waliokuwepo katika hafla hiyo fupi wameeleza matumaini yao kwa mgombea huyo na kuahidi kumpa ushirikiano katika safari ya maendeleo ya Jimbo hilo

Zoezi la kuchukua na kurudisha fomu linaendelea huku na likitarajiwa kufungwa rasmi Agosti 27,2025 huku wananchi wakisubiri kwa hamu kampeni na hatimaye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

GUSA LINK HAPA CHINI👇


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post