Na Lydia Lugakila, Ngara
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ngara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dotto Jasson Bahemu, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa kwa wananchi
kuelekea uchaguzi mkuu uajaofanyika Oktoba 29, mwaka huu akiahidi makubwa kwa Wana Ngara.
Bahemu amechukua fomu hiyo Agosti 26,2025 ambapo akiwa katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Ngara, Costantino Msemwa, amepokelewa na kukabidhiwa fomu hiyo rasmi tayari kukiwakilisha chama cha mapinduzi CCM.
Bahemu amepata ridhaa kutoka Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Ngara, baada ya kupita katika mchujo wa ndani ya chama na kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro hicho cha kisiasa.
Akizungumza baada ya zoezi hilo Bahemu amewashukuru viongozi wa chama pamoja na wananchi kwa kumuona kwa anafaa huku akiahidi kuwaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Ngara.
GUSA LINK HAPA CHINI👇
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment